Wednesday, April 20, 2011

Alhamisi kuu, siku ya kushiriki chakula cha Bwana

Huu ni muda wa kujikagua na kujichunguza na kutubu yale yatuzongayo yumkabidhi mana aliutoa uhai uhai wake kwaajili yangu mimi na wewe  1Petro 5:6-11

  Zaburi 25:1-5
"Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu , Nimekutumainia wewe nisiabike, Adui zangu wasifurahi kwa ............."


 1Korintho 11:23-38
"........kwa maana BWANA Yesu usiku ule alipotolewa aliutwaa mkate naye akiisha kushukuru akaumega akawapa wanafunzi wake akisema, huu ndio mwili wangu ulio kwaajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu............................."


                      
Mathayo 26:26-30
"...............................akautwaa mkate naye akiisha kushukuru akaumega akawapa wanafunzi wake akisema.....................sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa baba yangu, Nao walipokwisha kuimba , wakatoka nje kwenda mlima wa mizeituni.

MAOMBI
Tunakushukuru Mungu wa mbinguni kwaajili ya mwanao mpendwa Yesu Kristo ambaye ameutoa uhai wake kuwa dhabihu safi machoni pako kwaajili  yangu,ili mimi mwenye dhambi niweze kusafishwa mwili na roho na kuwa kiumbe kipya mbele zako,
Nakushukuru kwaajili ya damu yake inisafishayo na kuniondolea makosa yote,
Asante kwaajili ya jina lake ambalo linanilinda,
Nakushukuru kwa neema ya wokovu ninayoipata katika neno lake la uzima,
Asante kwa Roho wako mtakatifu aniongozaye,anifundishaye,anishauriye na kunisaidia katika kufanya maamuzi ya maisha yangu ili niweze kuishi maisha matakatifu.
Ninakuomba sasa BWANA unijalie kuishi maisha ya ukamilifu na imani ili niweze kuitunza neema hii ya wokovu na kufanikiwa na kubarikiwa katika maisha yangu .
A  M  E  N  I.

T.D. Jakes 9 calls out the conflict demon




T.D. Jakes 9 calls out the conflict demon, posted with vodpod

Prayer to Jesus

Oh BWANA YESU
Wewe uliye na moyo wa utii na unyenyekevu, naomba uniokoe kutoka kuabudiwa, kupendwa, kuinuliwa, kusifiwa, kukubalika kuliko wewe, kuaminiwa kuliko wewe, kuhesabiwa haki kuliko wewe, Uniondolee woga wa kunyanyasika, kudharauliwa, kusahaulika, kutofanikiwa, kugandamizwa, kuhisiwa, kukosea, kushutumiwa, kutokupendwa inavyostahili, kutoa maamuzi dhaifu yasio na ushindi bali nipe rehema za kutoa maamuzi yenye baraka kwa jamii na kwangu pia, Kwa rehema zako nijalie kubarikiwa ,kufanikiwa ,kuongezeka, kukubalika, kusikilizwa na  kuwa mtakatifu kama inavyostahili.
A  M  E  N  I
Maombi haya yatampa YESU nafasi yake katika maisha yako mana hakuna aliye na haki kuliko yeye, pia maombi haya yanatukumbusha kuwa tunahesabiwa haki kwa neema na imani na wala si kwa matendo ya sheria.