Oh BWANA YESU
Wewe uliye na moyo wa utii na unyenyekevu, naomba uniokoe kutoka kuabudiwa, kupendwa, kuinuliwa, kusifiwa, kukubalika kuliko wewe, kuaminiwa kuliko wewe, kuhesabiwa haki kuliko wewe, Uniondolee woga wa kunyanyasika, kudharauliwa, kusahaulika, kutofanikiwa, kugandamizwa, kuhisiwa, kukosea, kushutumiwa, kutokupendwa inavyostahili, kutoa maamuzi dhaifu yasio na ushindi bali nipe rehema za kutoa maamuzi yenye baraka kwa jamii na kwangu pia, Kwa rehema zako nijalie kubarikiwa ,kufanikiwa ,kuongezeka, kukubalika, kusikilizwa na kuwa mtakatifu kama inavyostahili.
A M E N I
Maombi haya yatampa YESU nafasi yake katika maisha yako mana hakuna aliye na haki kuliko yeye, pia maombi haya yanatukumbusha kuwa tunahesabiwa haki kwa neema na imani na wala si kwa matendo ya sheria.
No comments:
Post a Comment